Miradi yatakiwa kuhusishwa na tathmini za mazingira
5 August 2024, 6:21 pm
Wananchi wanaendelea kuhimizwa kutunzwa Mazingira ili yawatunze kwa kuepuka kufanya shughuli zinazoathiri Mazingira ikiwemo Kilimo na Ufugaji wa kuhama hama.
Na Mariam Kasawa.
Miradi mikubwa ya Kilimo endelevu inayoanzishwa imetakiwa kuhusishwa na tathmini za utunzaji wa Mazingira.
Kilimo kinatajwa kusaidia upatikanaji wa ajira nyingi Nchini huku uzalishaji wa Malighafi katika Viwanda mbalimbali unatokana na Mazao yatokanayo na Kilimo.
Uhusiano katika ya Kilimo na Mazingira upoje huyu hapa Naibu katibu mkuu wizara ya Kilimo Dkt. Hussein Mohamed Omar akieleza leo alipotembelea Banda la Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC.
Dkt. Careen Kahangwa Meneja NEMC Kanda ya kati anasema katika Miradi ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kuna Sheria ya Mazingira na kanunia ya tathmini ya Mazingira ambayo inataka Miradi hii kufanya tathmini za Kimazingira.