Jamii yatakiwa kuacha dhana potofu dhidi ya mafundi
2 August 2024, 6:02 pm
Pamoja na hayo Mafundi wamekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya uchumi, kiufundi na usalama wa Jamii hivyo ni muhimu Mafundi kuwa waaminifu ili kuhakikisha ufanisi na kiridhisha Wateja.
Na Witness.
Jamii imetakiwa kuachana na dhana potofu juu ya shughuli zinazofanywa na Wataalamu wa fani mbalimbali kuwa hawana uaminifu katika utekelezaji wa shughuli zao kwa Wateja.
Ufundi ni moja kati ya fani zinazotoa ajira kwa Vijana wengi Nchini, baadhi ya Vijana hukimbilia huko kwa ajili ya kujitafutia riziki zao za kila siku.
Ufundi umekuwa ni mbadala kwa Watu kujijiari, licha ya ustadi na umakini unaofanywa na baadhi ya Fundi hao, baadhi ya Watu husita kupeleka Vifaa vyao kwa Mafundi pindi vinapoharibika kwa kuohifia kuharibiwa zaidi au kuwekea vipuli bandia.
Nidhamu ya kazi na uaminifu ni msingi wa mafanikio katika kila unalolifanya na kuvutia Watu wengi, Mafundi wanazungumziaje dhana hii iliyopo juu yao.
Kwa wanaochafua fani hii ya ufundi wito unatolewa juu yao.