Dodoma FM

Kampeni za usafi zawahamasisha wananchi kusafisha mazingira Dodoma

31 July 2024, 6:22 pm

Picha ni wananchi wakifanya usafi wa mazingira katika moja ya mitaa hapa Jijini Dodoma.Picha na Mariam Kasawa.

Wananchi wametakiwa kutii sheria bila shuruti kwa sababu sheria ndogo ya usafi katika Jiji la Dodoma inasema mtu asipojitokeza kwenye usafi, asipofanya usafi kwenye eneo lake la makazi, taasisi na biashara, faini yake ni kati ya shilingi 50,000-200,000 au kifungo kisichozidi miezi sita au vyote viwili kwa pamoja.

Na Mariam Kasawa.
Kampeni za usafi zinazoanzishwa na Halmashauri ya Jiji la Dodoma zimetajwa kuwahamasisha Wananchi na Wafanyabiashara kufanya usafi katika Mazingira yao.

Kampeni ya mita tano usafi wangu, usafi wangu mita tano ilizunduliwa katika Jiji la Dodoma mnamo Januari 22 2022 kwa lengo la kuhamasisha Wananchi kufanya usafi wa Mazingira katika maeneo yao.
Wananchi wanasema kampeni za usafi zinasaidia kuwakumbusha Wanajamii kuwa jukumu la usafi ni la kila Mwananchi na linapaswa kufanyika kila wakati ili kuweka Mazingira katika hali ya usafi.

Sauti za wananchi.

Muhamasishaji wa vikundi vya usafi amewataka Wananchi kuendelea kufanya usafi katika maeneo yanayowazunguka ili kuendelea kuuweka Jiji katika hali ya usafi.

Sauti ya muhamasishaji vikundi vya usafi.

Mkuu wa Idara ya Mazingira na udhibiti wa taka ngumu wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dickson Kimaro amewataka Wananchi kuendelea kuitekeleza kampeni ya Mita tano usafi wangu, usafi wangu mita tano ili Mazingira yaendelee kuwa safi .

Sauti ya Dickson Kimaro .