Dodoma FM

Jamii yakumbushwa kumpa nafasi mwanamke

29 July 2024, 6:45 pm

Upo umuhimu wa jamii kutambua kuwa wanawake wana nafasi ya kuchangia wimbi la maendeleo katika ngazi ya familia hadi taifa. Picha na BBC.

Nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dkt. Samia Suluhu Hassan ni maono mema yenye kubeba taswira ya mabadiliko kwa jamii kutambua wanawake wanaweza kuongoza.

Na Victor Chigwada.
Jamii imekumbushwa kuona umuhimu wa kumpa nafasi mwanamke kwenye nyanja tofauti ili kuwezesha upatikanaji wa maendeleo.

Wito huo umetolewa na Afisa Maendeleo ya Jamii, kata ya Msamalo Bi.Ngw’ashi Mhuli ambapo amesema kuwa upo umuhimu wanawake kutambua kuwa wana nafasi ya kuchangia wimbi la maendeleo katika ngazi ya familia hadi taifa.

Akizungumza na Taswira ya Habari Ngw’ashi amesema kuwa uwepo wa Rais Dkt. Samia itaongeza chachu kwa wanawake kuwa na ujasiri na nafasi ya kushiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo.

Sauti ya Bi. Ngw’ashi Mhuli.

Leah Nathan ni mjumbe wa kikundi cha Tusaidiane amesema wanawake hivi sasa wana uwezo wa kufanya vizuri tofauti na mitazamo hasi iliyokuwa inafikiriwa hapo mwanzoni.

Sauti ya Bi. Leah Nathan.