Dodoma FM

Vijana watakiwa kuchangamkia fursa za kiuchumi zitokanazo na uchaguzi

24 July 2024, 4:19 pm

Picha ni Daglas Saidi ni Mtaalamu wa masuala ya uchumi.Picha na Fred Cheti.

Ni fursa zipi za kiuchumi ambazo vijana wanaziona katika chaguzi zijazo na zinazoweza kuwanufaisha.

Na Fred Cheti.
Vijana wameshauriwa kuzichangamkia fursa za kiuchumi kwa njia halali ambazo zitatokana na ujio wa chaguzi zijazo ikiwemo uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu pamoja na uchaguzi mkuu mwakani.

Rai hiyo imetolewa leo na Mwenyekiti wa Kamati ya habari kutoka jukwaa la Vijana Tanzania (Tanzania Youth Forum) wakati akifanya mahojiano na Dodoma TV ikiwa ni maandalizi ya Jukwaa la Vijana Tanzania kwa mwaka 2024 lenye kauli mbiu isemayo “Vijana kushiriki katika Uongozi, Utawala na mageuzi ya kiteknolojia kwa maendeleo ya kiuchumi.”

CLIP 1…..MWENYEKITI WA JUKWAA LA VIJANA

Picha ni kijana wa mtaa wa Swaswa akiongea na Dodoma Tv kuhusu fursa za kiuchumi zinazo jitokeza wakati wa uchaguzi.Picha na Fred Cheti.

Taswira ya Habari imezungumza na baadhi ya Vijana Jijini hapa,na kuhoji ni fursa zipi za kiuchumi ambazo wanaziona katika chaguzi zijazo na zinazoweza kuwanufaisha?

CLIP 2…..VIJANA JIJINI DODOMA MAONI UCHUMI

Daglas Saidi ni Mtaalamu wa masuala ya uchumi anasema kuwa kijana anaweza kubadilisha Mazingira yaliyopo kwa wakati husika na kuwa fursa za kiuchumi.

CLIP 3……MTAALAMU WA MASUALA YA UCHUMI