Dodoma FM

Matumizi sahihi ya ARV yanasaidia kuboresha afya

18 July 2024, 4:24 pm

Picha ni Dkt. Janet Mtenga kutoka kitengo cha kuhudumia watu wanaoishi na maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi. Picha na Yussuph Hassan.

Dkt. Janet Mtenga ameshauri jamii kujenga utamaduni wa kupima VVU na kutumia kwa usahihi dawa za kufubaza virusi vya ukimwi ARVs.

Na Yussuph Hassan.
Imeelezwa utumiaji kwa usahihi matumizi ya dawa za kufubaza Virusi Vya Ukimwi ARV inasaidia kuboresha afya na kuondoa uwezekano wa VVU kuwa sugu.

Kumekuwa na changamoto kwa baadhi ya watumiaji wa ARV kutotumia dawa hizo kwa wakati au kukatisha baada ya muda fulani na kusababisha kupata changamoto za kiafya.

Aisha Juma (siyo jina lake halisi) mpokea huduma katika kituo cha afya Makole amegundulika kuwa na maambukizi miaka tisa iliyopita anaelezea maisha yake kwa sasa.

Sauti ya Bi. Aisha Juma.

Dkt. Janet Mtenga kutoka kitengo cha kuhudumia watu wanaoishi na maambukizi ya VVU anaelezea umuhimu wa matumizi sahihi ya ARVs.

Sauti ya Dkt janet Mtenga .