Wasomi watakiwa kuwa mfano bora utunzaji wa mazingira
18 July 2024, 3:19 pm
Vijana ni nguvu kazi ya taifa hivyo wanatakiwa kutambua wajibu wao katika kutunza na kuhifadhi mazingira pia kuwa mabalozi wazuri wa mazingira.
Na Mariam Kasawa
Vijana wa vyuo vikuu wametakiwa kutunza mazingira kwa kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo upandaji miti na uanzishaji wa bustani za maua ili kuufanya Mkoa wa Dodoma kuwa mahali salama pa kuishi .
Sera ya Taifa ya Mazingira ya 1997 imeainisha changamoto sita ambazo ni; uharibifu wa ardhi; uharibifu wa misitu, kupotea kwa makazi ya viumbe-pori nabioanuai, kukosekana kwa maji salama mjini na vijijini.
Kupungua kwa ubora wa mifumo ya maji na uchafuzi wa mazingira hasa katika maeneo ya mijini na vijijini.
Changamoto hizi zinachangia kuzorotesha ukuaji wa uchumi na juhudi za serikali katika kupunguza umaskini na hivyo kuathiri maisha na ustawi wa jamii, Nimezungumza na Vijana wa vyuo vikuu kufahamu kama wanatambua wajibu wao katika utunzaji wa mazingira.
Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004 imeeleza wazi wajibu na majukumu ya wadau mbalimbali kuanzia serikali za mitaa hadi taifa katika Sheria hii ni mipango na usimamizi wa matumizi endelevu ya mazingira kudhibiti uchafuzi wa mazingira utunzaji wa taarifa na takwimu za mazingira.
Aloyce Kamando ni balozi wa mazingira kutoka ofisi ya Makamu wa rais yeye anasema vijana ni tegemeo la Taifa hivyo wanapaswa kutumia elimu yao katika kuunga mkono juhudi za Serikali katika utunzaji wa mazingira.