Watoto wanaoishi mazingira magumu hatarini matumizi ya gundi, tumbaku na petrol
18 July 2024, 2:37 pm
Picha ni Dkt. Christian Bwasi Afisa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya. Picha na Mindi Joseph.
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya haitafumbia macho wauzaji wazalisha na wafadhili wa dawa za kulevya kwani wanaua nguvu kazi ya taifa.
Na Mindi Joseph.
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya imeeleza kuwepo kwa wimbi kubwa la watoto wanaoishi katika mazingira magumu na hatarishi kutumia gundi, petroli na mazalia ya tumbaku.
Dkt. Christian Bwasi Afisa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya anabainisha hayo huku akieleza athari wanazopata watoto hao.
Afisa Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na Dawa za Kulevya kanda ya Kati Anna Tengia anabainisha kuwa dawa za kulevya hazikubaliki na wamekuwa wakichukua hatua kusaidia watoto hao.