Dodoma FM

Leo tunaangazia utoaji wa taarifa kuhusu vitendo vya ukatili wa kijinsia

15 July 2024, 5:58 pm

Kamanda Malya Akitambulisha kampeni ya ”FAMILIA YANGU HAINA MHALIFU” amesema kuwa jeshi la polisi limejipanga kuendelea kutoa elimu juu Ukatili uliokithiri.Picha na Google.

Amewataka wanafunzi hao kuepuka matendo maovu.

Na; Mariam Matundu.
kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Dodoma na Kamishina Msaidizi mwandamizi wa Polisi SAPC Theopista Mallya imeitaka jamii kukemea vitendo vya ukatili kwa kutoa taarifa ya vitendo hivyo katika jeshi la polisi .

Akizungumza na wanafunzi wa Kidato cha kwanza hadi cha Sita katika shule ya wasichana Huruma Jijini Dodoma, amewataka wanafunzi hao kuepuka matendo maovu, kuripoti matukio mabaya yanayojitokea katika jamii huku akiwataka wawe mabalozi kwa kuishi maadili mema.

Aidha Kamanda Malya Akitambulisha kampeni ya ”FAMILIA YANGU HAINA MHALIFU” amesema kuwa jeshi la polisi limejipanga kuendelea kutoa elimu juu Ukatili uliokithiri, ikiwepo mauaji,ubakaji, ulawiti na usagaji na mmomonyonyo wa maadili ulikithiri ili kuondoa kabisa uhalifu katika jamii ya watanzania.