Serikali kuchimba visima Igandu zaidi ya vitatu
15 July 2024, 5:29 pm
Hata hivyo Serikali kupitia RUWASA bajeti ya 2023/2024 imepanga kujenga jumla ya miradi 1546.
Na Victor Chigwada.
Matumaini ya kupata huduma ya maji safi na salama yameanza kupata nuru kwa wananchi wa Kata ya Igandu baada Serikali kutenga fedha za kuchimba visima zaidi ya vitatu.
Hatua hiyo inakuja ikiwa Huduma ya maji safi na salama imekuwa changamoto kwa wakazi hao kwa kipindi kirefu hali iliyosababisha wananchi kutumia maji yasio safi na salama na kuhataraisha afya zao
Baada ya serikali kuchukua hatua ,Taswira ya Habari imezungumza na Wakazi wa Igandu ambapo wameishukuru Serikali kupitia wakala wa maji vijijini RUWASA kwajitihada za kumtua ndoo kichwani mwanamke.
Wakielezea hali ilivyokuwa hapo mwanzoni ,baadhi yao wamesema kuwa walilazimika kuamka alfajiri ili kuwahia katika kutafuta maji.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Igandu John Nhugutu amekiri uwepo wa changamoto hiyo uliochangiwa na uwepo wa kisima cha maji ambacho kilikuwa na wingi wa chumvi.
Akizungumza hatua ya Serikali ya kutatua changamoto hiyo amesema tayari wamepokea milioni mia nne kwa ajili ya uchimbaji wa Visima vya maji.