Dodoma FM

Wanao safirisha watoto mijini kufanya kazi waonywa kuacha mara moja

8 July 2024, 5:32 pm

Picha ni Bi. Jane Mgidande mratibu wa elimu Jumuishi kutoka shirika la FPCT .Picha na Mariam Kasawa.

Kwa mujibu wa sheria ya Ajira na Mahusiano ya Kazi ya mwaka 2004 inasema ni kosa kuajiri watoto kinyume na sheria ya kazi inavyosema na adhabu inatolewa chini ya kifungu cha 102 (2) ambacho kinampaHakimu wa Wilaya na Mkazi kutoa adhabu sawa na faini isiyozidi shilingi milioni 5 au kifungo cha mwaka mmoja au vyote faini na kifungo kama mahakama itavyoona inafaa.

Na Mariam Kasawa.
Wazazi wameonywa kuacha tabia ya kuwashinikiza watoto hususani wakike kuacha masomo au kujifelisha ili wakafanye kazi za ndani.

Katika kata ya Bahi baadhi ya wazazi wamekuwa na tabia ya kuwakatisha watoto masomo yao na kuwapeleka mjini wakafanye kazi za ndani wasaidie familia .

Afisa maendeleo kata ya Bahi amesema katika Mkoa wa Dodoma eneo la Chimendeli na Mpamantwa ndio yanaongoza kupeleka watoto mjini kwenda kufanya kazi za ndani hivyo amewataka wazazi kuacha hii tabia kwani wakibainika adhabu kali itachukuliwa dhidi yao.

Sauti ya Afisa maendeleo ya jamii.
Picha ni Wakazi wa Kijiji cha Uhelela wakiwa katika kikao .Picha na Mariam Kasawa.

Nae Bi. Jane Mgidande mratibu wa elimu Jumuishi amewataka wazazi kuacha tabia ya kuwakatisha watoto wa kike masomo kwani wanawanyima fursa mbalimbali wanapokosa elimu.

Sauti ya Bi. Jane Mgidange.

Kwa upande wake mratibu wa elimu kata ya Bahi yeye amesema tayari wameanza kufuatilia watoto wote ambao waliacha ambapo amewataka watoto wote walio acha shule kujisalimisha shuleni haraka.

Sauti ya Mratibu Elimu kata ya Bahi.