Dodoma FM

Wazazi watakiwa kuwapatia watoto haki ya kupata elimu

8 July 2024, 4:23 pm

Mratibu elimu kata ya Bahi akiongea na wakazi wa kijiji cha Uhelela. Picha na Mariam Kasawa.

Sera ya elimu jumuishi imekuwa mkombozi kwa watoto wote kufurahia elimu pamoja.

Na Mariam Kasawa.
Wazazi wametakiwa kutambua kuwa haki ya kupata elimu ni yakila mtoto hivyo wanapaswa kuwaacha watoto wasome na kuwapatia mahitaji yote muhimu.

Sera ya elimu jumuishi imekuwa mkombozi kwa watoto wote kufurahia elimu pamoja baadhi ya wazazi walio kuwa wamewakatia tamaa watoto wao wenye ulemavu wanasema kwasasa wanajivunia elimu jumuishi kwani watoto wanapata nafasi ya kusoma na kujifunza vitu mbalimbali.

Sauti za wazazi.

Nae Diwani wa kata ya Bahi Bw. Augustino Ndunu amewataka wazazi wote wenye watoto wenye ulemavu wajitahidi kuwapatia mahitaji yao ya msingi ikiwemo kuwapeleka shule kupata elimu.

Sauti ya Bw. Augustino Ndunu .