Dodoma FM

Watu wenye ulemavu watakiwa kuungana na serikali kupinga vitendo vya ukatili

25 June 2024, 6:33 pm

Udhibiti wa vitendo hivyo vya ukatili unahitaji nguvu ya pamoja. Picha na Mindi Joseph.

Tayari serikali imejenga mifumo thabiti ya udhibiti wa vitendo hivyo na kilichobaki ni ushiriki wa makundi yote ya jamii katika kuhakikisha vitendo hivyo viovu vinakomeshwa hapa nchini.

Na Mindi Joseph.
Watu wenye ulemavu wametakiwa kuungana na serikali katika mapambano dhidi ya vitendo vya kikatili vinavyofanywa na baadhi ya watu kwa kundi la watu wenye ulemavu na vinavyorudisha nyuma Maendeleo yao.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Foundation For Disabilities Hope Michael Salali anasema udhibiti wa vitendo hivyo unahitaji nguvu ya pamoja.

Sauti ya Michael Salali.

Katika Hatua nyingine amewaomba Wakuu wa Mikoa na wilaya kufanyia kazi maagizo yaliyotolewa na Waziri Mkuu kassim Majali ili kutatua tatizo hilo.

Sauti ya Michael Salali.

Hivi karibuni Waziri Mkuu Kasim Majaliwa aliziagiza Mamlaka za Mikoa na Wilaya zihamasishe ushiriki wa jamii katika ulinzi na haki za watu wenye ualbino kwani vitendo vya mauaji ya albino vinahusisha mtandao wa watu na siyo mtu mmoja mmoja.

Sauti ya mh. Kasim Majaliwa.