Dodoma FM

Jamii yatakiwa kuwasilisha migogoro ya bima TIO

13 June 2024, 12:41 pm

Bw. Aloyce Mbunito Msuluhishi Mwandamizi kutoka ofisi hiyo ya Usuluhishi wa Migogoro ya bima  (TIO).Picha na Fred Cheti.

Ofisi ya Msuluhishi wa migogoro ya bima ni taasisisi inayojitegemea iliyoanzishwwa chini ya sheria ya bima Namba 10 YA MWAKA 2009 sura 394 na ilianza kufanya kazi mwaka 2015 baada ya msuluhishi kuteuliwa.

Na Fred Cheti.

Jamii imetakiwa kuwasilisha Migogoro yoyote ya bima katika ofisi ya Msuluhishi wa migogoro ya bima (TIO) ili iweze kutatuliwa kwa njia mbadala nje ya utaratibu wa kawaida wa kimahaka.

Hayo yameelezwa na bwana Aloyce Mbunito Msuluhishi Mwandamizi kutoka ofisi hiyo ya Usuluhishi wa Migogoro ya bima  (TIO) wakati akizungumza katika kipindi cha The Morning Power show kuelezea majukumu ya ofisi hiyo ambapo amesema moja ya malengo ya ofisi hiyo ni pamoja na kumlinda mtumiaji wa bima ili kukuza na kujenga imani kwa umma katika biashara ya bima .

Sauti ya bwana Aloyce Mbunito.

Kwa upande wake Mkaguzi wa Nyaraka za migogoro ya bima kutoka ofisi ya Msuluhishi wa migogoro ya bima Mariamu Mkuja anaeleza ni nyaraka zipi mlalamikaji inabidi awe nazo ili aweze kupatiwa huduma.

Sauti ya Bi Mariam Mkuja.