Dodoma FM

UCSAF wapongezwa kwa kusimamia vema dhamana waliyopewa

15 May 2024, 12:36 pm

Picha ni wakazi wa Kata ya Namelock wilayani Kiteto wakiwa katika mkutano wakati wa uzinduzi wa mnara .Picha na Mariam Kasawa.

Mnara huu ulio kaguliwa na Waziri Nape umegharimu kati ya milioni 300 mpaka milioni 350 na ni moja kati ya Minara 758, ambayo Ujenzi wake unatekelezwa katika maeneo mbalimbali hapa Nchini.

Na Mariam Kasawa.

Mfuko wa mawasiliano kwa wote (UCSAF) umepongezwa kwa kazi nzuri unazofanya wa kuhakikisha unasaidia ujenzi wa minara sehemu ambazo makampuni ya simu hayawezi kupeleka minara kwa sababu za kibiashara.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari, mawasiliano ya teknolojia ya Habari Nape Nauye alipofanya ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa mnara Wilayani Kiteto Mei 13, 2024 ambao ni miongoni mwa minara 758 ambayo ilitiwa saini mwaka 2023.

Waziri Nape ameishukuru kampuni ya simu ya Airtel kwa kuongoza katika ukamilishaji wa minara ya mawasiliano tofauti na kampuni zingine za simu.

Sauti ya Mh. Nape Nauye.
Picha ni Waziri wa Habari, mawasiliano ya teknolojia ya Habari Nape Nauye akiwa pamoja na viongozi wengine baada ya kuvalishwa vazi la kimila na wazee wa kimasai katika mkutano huo.Picha na Mariam Kasawa.

Nae Mbunge wa Jimbo la Kiteto Edwarg Ole Lekaita akiongea wakati wa hafla hiyo amesema kilio cha wakazi wa kata ya Namelock kwa muda mrefu ilikuwa ni kupata mnara kwa ajili ya mawasiliano ya simu.

Sauti ya Mh. Edward Lekaita.

Akiongea kwa niaba ya mkurugenzi Mkuu wa Airtel meneja wa Airtel kanda ya kati amesema wataendelea kushirikiana na serikali pamoja na wizara husika kupanua wigo wa mawasiliano ndani ya Nchi.

Sauti ya meneja wa Airtel kanda ya kati