Endeleeni kuitekeleza kampeni ya mita tano usafi wangu usafi wangu mita tano
19 March 2024, 6:20 pm
Kimaro amewataka wananchi kutii sheria bila shuruti kwani sheria ndogo ya jiji la Dodoma inasema mtu asipo jitokeza kwenye usafi wa eneo lake la makazi , taasisi na biashara, faini yake ni kati ya shilingi 50,000-200,000 au kifungo kisichozidi miezi sita au vyote viwili kwa pamoja.
Na Mariam Kasawa.
Wakazi wa Jiji la la Dodoma wametakiwa kuendelea kutekeleza kampeni ya ‘mita tano usafi wangu, usafi wangu mita tano’kwa kufanya usafi katika mazingira ya nyumba na ya biashara.
Viongozi wa serikali mitaa wanaitekelezaje kampeni hii ili ilete tija kwa jiji la Dodoma huyu hapa Bw. Ally Yasin mwenyekiti wa mtaa wa Sokoine akieleza.
Mnamo jan 22 mwaka 2022 kampeni ya mita tano usafi wangu , usafi wangu mita tano ilizinduliwa katika kata ya Makole Jijini Dodoma na aliye wahi kuwa mkurugenzi wa jiji la Dodoma wakati huo bwana Joseph Mafuru .
Aliwasihi wananchi kuendeleza tabia ya usafi ili kuijenga kuanzia kwa wazazi hadi watoto kwa kizazi kilichopo na kijacho.
Utekezaji wa kameni hii upoje kwa sasa baada ya kuzinduliwa miaka miwili iliyopita huyu hapa Mkuu wa Idara ya Mazingira na udhibiti wa taka ngumu wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dickson Kimaro akieleza.