Baadhi ya wafanyabiashara pamoja na madereva wanasema kuwa mabasi kutokuingia ndani ya kituo hiki ni kutokana na miundombinu mibovu. Picha na Thadei Tesha.
Mbali na shughuli za kuuza na kununua bidhaa [pamoja na usafiririshaji kushamiri hapa lakini kituo hiki kidogo cha mabasi bado kinaonekana kuwa na mashimo makubwa na madimbwi ya maji jambo linaloweza kusababisha athari kwa vyombo vya usafiri kuharibika.
Na Thadei Tesha.
Biashara na shughuli ndogondogo zinazofanyika katika kituo cha Mnada Mpya jijini Dodoma zimeendelea kufanyika kwa shida kutokana na uwepo wa changamoto mbalimbali ikiwemo miundombinu na magari kutoingia ndani ya kituo.
Katika eneo la Mnada Mpya jijini Dodoma shughuli mbalimbali za kutafuta riziki zinaendelea hapo, wapo madereva bodaboda, machinga lakini pia wapo akina mama wanaofanya biashara ndogondogo.
Baadhi ya wafanyabiashara pamoja na madereva wanasema kuwa mabasi kutokuingia ndani ya kituo hiki pamoja na miundombinu mibovu imepelekea wengi wao kukosa wateja.
Pamoja na madereva na wafanyabiashara hawa kulalamikia changamoto hii ombi kubwa kutoka kwa wafanyabiashara hawa ni kuwataka viongozi wa juu kuwatembelea na kuskiliza kero zao.
Lakini je mamlaka zinazungumziaje changamoto ya magari kutoingia ndani ya kituo hiki? Huyu hapa ni afisa Mfawidhi LATRA jiji la Dodoma Bw Ezekiel Emmanuel anatolea majibu.