Wakazi wa Bicha Kondoa wahofia kuathirika na mafuriko
27 December 2023, 4:58 pm
Wananchi wanaoishi pembezoni mwa mkondo wa maji wamekuwa wakisisitizwa kuhama maeneo hayo ili kuepuka athari ambazo zinaweza kuwapata ikiwemo ikiwemo mvua kubwa zinazoambatana na uharibifu wa mali na maisha ya watu.
Na Nizar Mafita.
Wananchi wa Mtaa wa Bicha katika halmashauri ya mji kondoa waishio katikakingo za bwawa la bicha wapo hatarini kuathirika na mafuriko yanayoweza kutokea kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
imezungumza na baadhi ya wananchi wanaoishi jirani na maeneo hayo na kueleza juu ya usalama wao hasa kipindi cha mvua.
Wananchi hao wamesema sirahisi kufikiwa na maji ya bwawa hilo kutokana na wao wapo katika mwinuko licha ya kwamba wanaishi umbali wa mita 25 kutoka usawa wa bwawa.
Mtaalamu wa ardhi na mswala ya mipango miji kutoka kondoa Alibashiru Issa amewataka wananchi kujiridhisha juu ya maeneo sahihi ya kuweka makazi kwa kufika katika ofisi za mipango miji ili kuepuka athari ambazo zinaweza kutokea.
Idd abdalah ramadhan mwenyekiti wa mtaa wa biocha amezungumza na kituo hiki na kuwataka wananchi waishio maeneo ya pembezoni mwa bwawa la bicha kuchukua tahadhari mapema kabla ya kutokea maafa.