Mabadiliko ya bei kuongeza upatikanaji wa maji Dodoma
15 August 2023, 9:55 am
Ongezeko hilo la bei za maji limechangiwa kwa kiasi kikubwa na mabadiliko ya kiuchumi duniani.
Na Selemani Kodima.
Baada ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) Kuweka wazi mabadiliko ya bei za huduma za maji zitakazoanza kutumika mwezi August mwaka huu ,Inaelezwa kwa mabadiliko hayo ambayo yatatekelezwa kwa miaka mitatu yasaidia kuongeza hali ya Upatikanaji wa maji mkoani Dodoma.
Hayo yamesemwa Leo na Mkuu wa Kitengo cha Mipango ,Tathimini na Ufuatiliaji (DUWASA)Jonathan Shenyagwa wakati akizungumza katika kipindi cha Dodoma Live kuhusu mabadiliko ya bei mpya za huduma za maji ambapo amesema kupitia Bei hizo kwa asilimia 90 wanategemea kupunguza Tatizo la Mgao wa maji katika jiji la Dodoma.
Akizungumza kuhusu Ankara mpya ,zenye mabadiliko ya Bei za huduma ya Maji,Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja Bi ,Lena Mwakisale amesema bei mpya zitaanza kutumika mwishoni mwa mwezi huu ,tarehe 24 Agosti ambapo mabadiliko hayo yameongezeka kidogo.
Amesema ukitazama kwenye kila kundi la Wateja kilichoongeza ni Shilingi 200 kwa kila unit ambapo kwa Wateja wa Majumbani itakuwa Shilingi 1510 ,Wateja wa Taasisi 1880,Wateja Biashara 1930 ,Wateja Viwanda 1930 ,wateja wa Magati 1000 na Wateja wa Jumla 2000.
Amesema kwa Mwaka 2024/2025 itakuwa tofauti ambapo Wateja wa Majumbani itakuwa Shilingi 1650 ,Wateja wa Taasisi 2050 ,Wateja Biashara 2100,Wateja wa Viwandani 2100 na Wateja Wakubwa 2060
Kwa upande Mwingine Mkuu wa Kitengo cha Mipango na Tathimini na Ufuatiliaji Bw Shenyangwa amesema baada ya Mabadiliko hayo ya bei ,DUWASA ina mkakati kutoa Huduma endelevu kwa wakazi wa Dodoma na kupitia miradi inayotekelezwa ya uchimbaji wa Visima vya maji katika maeneo ya pembezoni itaongeza hali ya upatikanaji wa maji jijini Dodoma.
Amesema moja ya Mradi unaotegemewa kuongeza hali ya Uzalishaji wa maji katika maeneo ya jiji la Dodoma ni pamoja na mradi wa visima vya Maji nzuguni ambao upo hatua za Mwisho kukamilika ili kuanza kutoa maji.
Kwa mujibu wa EWURA imetaka kila Mamlaka kupitia bei zake kila baada ya miaka Mitatu na DUWASA haikua imefanya hivyo katika kipindi hicho huku moja ya sababu ilitojwa kusukuma mabadiliko hayo ni kuwezesha Mamlaka kumudu gharama za uendeshaji, kuongeza ufanisi wa DUWASA katika utoaji wa huduma bora, kuimarisha na kuboresha usalama wa maji yanayozalishwa na kusambazwa.