NIDA yatoa vitambulisho 62,258 Kongwa
17 May 2023, 3:03 pm
Changamoto wanazopitia wananchi katika vitambulisho vya Taifa ni pamoja na kushindwa kutimiza vigezo na masharti ya kujaza fomu za kuomba vitambulisho hivyo hali inayopelekea ofisi kushindwa kufanya kazi yake kwa ufanisi.
Na Bernadetha Mwakilabi.
Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA) wilaya ya Kongwa imepokea vitambulisho vya Taifa 62,258
Akiongea katika mkutano wa hadhara Kijiji cha Pingalame kitongoji cha Subugo Afisa usajili wilaya ya Kongwa bwana Said Hamad amesema wamepokea vitambulisho hivyo mwezi Mei ambapo vitambulisho hivyo vitaanza kugawiwa kwa wananchi vijijini muda wowote kuanzia Jumatatu ya tarehe 22 mwezi huu.
Aidha Hamad amewasihi wananchi katika Kila Kijiji kufatilia matangazo yatakayotolewa katika maeneo yao juu ya nàmna ya kuchukua vitambulisho hivyo.
Hamad ameongeza kuwa kumekuwa na changamoto nyingi wanazokutana nazo katika kuwasajili wananchi katika vitambulisho vya taifa ikiwemo wananchi kushindwa kutimiza vigezo na masharti ya kujaza fomu za kuomba vitambulisho Hali inayopelekea ofisi kushindwa kufanya kazi yake Kwa ufanisi.
Sambamba na hayo Hamad amejibu malalamiko ya hivi karibuni yaliyotolewa na wananchi hususani wa kata ya Kibaigwa juu ya kuchelewa Kwa vitambulisho vya taifa.
Katika maelekezo yake mkuu wa wilaya Kongwa Mheshimiwa Remidius Mwema Emmanuel ameagiza wàtendaji wa vijiji kuandaa orodha ya wananchi ambao bado hawajapata vitambulisho na ambao wapo kwenye mchakato ili ofisi ya usajili ishughulikie.