Wanafunzi watembea zaidi ya kilomita 28 kufuata shule
28 February 2023, 5:21 pm
Serikali imeombwa kusaidia kukamilisha ujenzi wa shule ya sekondari ili kurahisha upatikanaji shule hali itakayopunguza gharama kwa wazazi wanaosomesha watoto .
Na Victor Chigwada
Wanafunzi wa kata ya chiboli wilayani chamwino wanalazimika kutembea umbali wa zaidi ya km 28 kila siku kwaajili ya kwenda shule ya sekondari Fufu.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa kijiji cha Champumba Bw.John Mdabaji ambapo amesema kuwa kutokana na adha ya umbali huo wamejaribu kujenga baadhi ya vyumba vya madarasa ambavyo bado havijakamilika kwa kutumia nguvu za wananchi
Naye Diwani wa Kata ya Chiboli Bw.Wiliamu Teu amesema kuwa wameendelea na juhudi za ujenzi wa sekondari na kuwaomba wadau pamoja na Serikali kuwasaidia kukamilisha ujenzi huo
Teu ameongeza kuwa changamoto ya kilomita 28 za kufuata elimu ya sekondari imekuwa ikiongeza gharama za kimaisha kwa wazazi hususani wale wa hali ya chini