Dodoma FM

Umbali mrefu wa kufika shule wapelekea wanafunzi kuacha shule.

31 January 2022, 3:19 pm

Na; Neema Shirima.

Imeelezwa kua umbali mrefu wa kufika shuleni umekuwa ni chanzo cha utoro kwa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Zuzu.

Hayo yamesemwa na baadhi ya wananchi wa mtaa wa Chididimo katika kata ya Zuzu ambapo wamesema inawalazimu wanafunzi kutembea umbali mrefu kwa ajili ya kwenda shuleni hali inayochangia baadhi yao kushindwa kuendelea na masomo

Clip 1…..wazazi

Aidha kwa upande wa wanafunzi hao wamesema inawalazimu kuamka saa kumi na moja alfajiri na kufika saa mbili na nusu hadi saa tatu shuleni na kusema kuwa wakati mwingine hua wanakutana na wanyama wakali njiani jambo ambalo ni hatari kwa maisha yao

Clip 2……wanafunzi

Nae mwenyekiti wa mtaa huo bwana Boniface Laurent amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo ambapo amesema hadi sasa ni wanafunzi saba tuu walioripoti shuleni kati ya wanafunzi sitini na tatu waliochaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari ambapo bado wanaendelea kuwafuatilia kuhakikisha wote wanaripoti shuleni

Clip 3…..mwenyekiti

Ni jukumu la kila mzazi pamoja na serikali kuhakikisha wanafunzi wanakuwa salama katika mazingira yanayowazunguka ili kuwalinda na vishawishi ambavyo vinaweza kuwapelekea kukatisha ndoto zao