Wizara ya nishati imetakiwa kuhakikisha kunakuwepo na umeme wa kutosha ili kuwezesha sekta ya uchimbaji madini
28 October 2021, 9:48 am
Na; Shani Nicolous.
Tanzania inatarajia kutengeneza ajira milioni 987 Kutokana na ubia muendelezo na makampuni ya Madini.
Akizungumza na Taswira ya habari Waziri wa Madini Dotto Biteko amesema kuwa Tanzania inatarajia kutengeneza ajira milioni 987 na mapato ya Dola za marekani bilioni 7.54 sawa na fedha za Tanzania takribani Trilioni 17.35 Kutokana na ubia muendelezo na makampuni ya Madini.
Aidha amewataka wananchi kujiandaa kufanya uwekezaji katika sekta mbalimbali zitakazohudumia katika mgodi.
Nae Spika wa Bunge Job Ndugai ameitaka wizara ya nishati kuhakikisha kunakuwepo na umeme wa uhakika ili kuwezesha sekta ya uchimbaji madini nchini.
Akizungumza wakati wa hafla ya utoaji leseni ya uchimbaji mkubwa wa Madini kwa kampuni ya Tembo Nickel Corporation Limited na uzinduzi wa Taarifa ya Uhamasishaji,uwazi na uwajibikaji katika Rasilimali Madini,mafuta na gesi asilia (TEITI) ya mwaka 2018/19,amesema katika uchimbaji huo mkubwa ni muhimu kuwepo na umeme wa uhakika ili kutokwamisha shughuli hiyo.
Amesema kuwa awali ilikuwa ngumu sana kupitisha bajeti ya wizara ya Nishati na Madini kutokana na imani ya watanzania na wabunge kuwa ndogo sana kwenye sekta hii.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi jijini hapa wamesema imani yao nikupokea fursa lukuki kutoka katika wizara mbalimbali hasa madini hivyo serikali iendelee kukaribisha uwekezaji nchini ili kupunguza umaskini kwa baadhi ya wananchi.