Ukosefu wa elimu kwa familia ni kikwazo kwa mtoto wa kike
19 October 2021, 11:24 am
Na;Mindi Joseph.
Ukosefu wa elimu kwa familia imetajwa kuwa kikwazo kwa watoto wa kike kwani hushawishiwa na familia kufanya vibaya mitihani yao ya taifa ili waolewa na wazazi kuepuka kuwasomesha.
Akizungumza na Taswira ya habari Denis Komba Mkuu wa idara ya maendeleo ya Jamii wilaya ya bahi amebainisha kuwa bado kuna changamoto zinazowakabili watoto wa kike hali inayosababisha kutofanikisha kutimiza ndoto zao katika elimu.
Ameongeza kuwa Familia nyingi zimekuwa na mwamko mdogo kuhusu elimu kwani zinawaelekeza watoto wao kufanya vibaya katika mitihani yao.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Bahi Bw Augstino Ndonuu amesema baadhi ya wazazi wamekuwa na mwelekeo chanya kwa watoto wao wa kike na kuchangia ukatili kwa watoto hao.
Kufuatia Changamoto hiyo Wilaya ya Bahi imeendelea kushirikiana na wadau na mashirika mbalimbali ili kuwasaidia watoto wa kike kuepukana na changamoto hizo.