Wakazi wa Mpwayungu waaswa kuacha kuendekeza undugu katika masuala ya ukatili dhidi ya watoto na wanawake
7 October 2021, 12:16 pm
Na; Alfred Bulahya.
Wakazi wa kata ya Mpwayungu wilayani Chamwino mkoani Dodoma, wametakiwa kuacha kuendekeza undugu katika mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto na badala yake washirikiane na mamlaka zinazosimamia masuala hayo ili kukomesha vitendo hivyo.
Hayo yamebainishwa na Afisa maendeleo ya jamii kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa bi Honorata Rwegasira, wakati akizungumza na wajumbe wa kamati ya ulinzi wa mwanamke na mtoto (MTAKUWA) kwenye kikao maalumu kilichofanyika mapema leo katika kata hiyo.
Amesema suala la ulinzi wa mwanamke na mtoto linapaswa kutofumbiwa macho na kuacha kuendekeza udungu ambao umekuwa ukisababisha kushindwa kutolewa kwa ushahidi, kwa lengo la kulinda undugu uliopo baina ya mtenda na mtendewa.
.
Amesema Katika kikao hicho wamekubaliana na kuanza zoezi la kukutana kila baada ya miezi 3, kutoa elimu kwenye mikutano ya hadhara, lengo ni kukumbushana majukumu ya kamati ili kuendeleza mapambano hayo.
Baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo wamesema moja ya changmoo kubwa inayokwamisha juhudi hizo ni kikosekana kwa ushirikiano baina ya wazazi na watendaji hivyo ni wazi kuwa elimu inahitajika kuendelea kutolewa.
Nao baadhi ya wanafunzi wamewashauri wanafaunzi wenzao kuachana na tamaa za kutka kumiliki vitu vizuri wakiwa wadogo na kwamba waepuke kusikiliza maneno ya upotoshaji ambayo huchangia ongezeko la vitendo vya ukatili ikiwemo mimba na ndoa za utotoni.
Kikao hicho kilichofanyika katika kata hiyo kimeandaliwa na shikira la woman wake aup (WOWAP) na kimewakutanishwa wajumbe wa kamati hiyo inayoundwa na walimu wa shule za msingi na sekondari, watendaji wa kata na vijiji, polisi na wanafunzi wa shule za sekondari na msingi.