Umeme waathiri upatikanaji wa maji Membe.
4 October 2021, 2:34 pm
Na; Benard Filbert.
Kuchelewa kuwashwa kwa nishati ya umeme wa tanesco katika kata ya Membe wilayani Chamwino imetajwa kuathiri upatikanaji wa huduma ya maji kwa wakazi wa kata hiyo.
Hayo yameelezwa na diwani wa kata ya Membe bwana Simon Macheo wakati akizungumza na taswira ya habari kuhusu changamoto ya upatikanaji wa maji kwa baadhi ya maeneo ndani ya kata hiyo.
Bwana Macheo amesema kuna baadhi ya visima katika kata hiyo vina maji yakutosha lakini vinashindwa kutoa maji kutokana na ukosefu wa umeme hivyo tanesco wilaya ya Chamwino wamemaliza kutengeneza miundombinu yote ya umeme na hatua inayofuata ni kuwasha huku umeme huo ukitumika kutoa maji.
Akizungumzia kuhusu umeme kufika katika vijiji vyote vya Membe amesema vimebaki vichache lakini awamu itakayofuata itakamilisha zoezi hilo.
Huduma ya umeme katika kata ya Membe wilayani Chamwino inatarajiwa kuanza muda wowote kutoka hivi sasa mara baada ya kukamilika kwa uwekaji wa miundombinu ya umeme katika baadhi ya maeneo ya kata hiyo.