Dodoma FM

Vyombo vya ulinzi na usalama vyaagizwa kuchukua hatua za kisheria dhidi ya watu wanao tumia mitandao ya kijamii vibaya

16 September 2021, 2:01 pm

Na;Mindi Joseph .


Waziri wa Mambo y a Ndani ya Nchi George Simbachawene ameviagiza Vyombo vyote vya ulinzi na usalama Nchini kuanza kuchukua hatua za kisheria kwa wale ambao wanatumia mitandao ya kijamii vibaya ikiwemo kudhalilisha viongozi.
Akizungumza leo Mtumba Jijini Dodoma wakati wa Kikao Cha kazi na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama ambao wamekutana kujadili hali ya usalama wa Nchi pamoja na kujitathimini katika zana ya usalama.
Amebainisha kuwa wapo baadhi ya watu wanatumia uhuru wao wa mawazo vibaya na kukiuka kanuni na Sheria za Nchi hasa matumizi ya mitandao ya kijamii na kwamba kama Serikali haiwezi kukaa kimya hivyo lazima wachukue hatua.
Clip1..Simbachawene
Aidha amelitaka Jeshi la Polisi pamoja na Ofisi ya Mwendesha mashitaka wa makosa ya jinai Nchini Kamishina Cammillius Wambura DCI kuhakikisha wanaharakisha upelelelzi wa kesi za uhalifu wa kimtandao ili kupambana na suala hilo.
Clip2..Simbachawene
Katika hatua nyingine ameitaka Wizara ya mawasiliano kuendelee kushirikiana na Jeshi la Polisi ili wahusika wa makosa hayo ya kimtandao waweze kuchukuliwa hatua kwa haraka ikiwemo kufikishwa Mahakamani
Kwa mjibu wa Waziri Simbachawene Wizara hiyo inatarajia kuanzisha Kanda sita kwa ajiili ya uchunguzi wa Kimaabara kutokana na kesi za kimtandao na baada ya muda mfupi itakuwa ni historia.