Watoto wanaoishi na kufanya kazi mtaani wametajwa kuwa katika hatari ya kufanyiwa vitendo vya ukatili
13 September 2021, 1:21 pm
Na;Mariam Matundu.
Watoto wanaoishi na kufanya kazi mtaani wametajwa kuwa katika hatari ya kufanyiwa vitendo vya ukatili ikwemo kubakwa na kulawitiwa pamoja na kutumikishwa katika magenge yakihalifu.
Hayo yamesemwa na katibu mkuu wizara ya afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto idara kuu ya maendeleo ya jamii Dkt John Jingu katika kikao cha kujadili na kuweka mikakati ya kushughulikia tatizo la watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani .
Dkt Jingu amesema kupitia kikao kazi hicho kilichokutanisha wadau mbalimbali kitasaidia kupunguza changamoto zinazowakabili kundi hilo la watoto.
Aidha amesema watoto wanaoishi na kufanyakazi mitaani bado ni tatizo kubwa kwani kwa mujibu wa taarifa ya Tamisemi ya mwaka 2018 inaonesha idadi ya watoto 35919 wanaoishi na kufanya kazi mitaani katika majiji na miji mbalimbali hapa nchini .
Nae kaimu kamishina wa ustawi wa jamii wizara ya afya idara kuu ya maendeleo ya jamii Shirungu Ndaki amesema wizara inaendelea na jitihada kushughulikia changamoto za watoto ambapo hadi mwezi march mwaka huu 2021 watoto 1506 walitengamanishwa na familia zao .
Kwa upande wake mkurugenzi wa shirika la PACT TANZANIA Mariana Balampama amesema wamekuwa wakishirikiana vizuri na serikali katika kutoa huduma kwa watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi ambapo kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita zaidi ya watoto 8300 wamefikiwa.
Wadau mbalimbali wamekutana jiji Dodoma kwa siku mbili sept 13 na sept 14 ili kujadili na kuweka mikakati ya kushughulikia tatizo la watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani .