Kata ya Hogoro , wilayani Kongwa yakabiliwa na uhaba wa wodi za wazazi na upungufu wa wahudumu wa Afya
9 August 2021, 1:31 pm
Na ;Victor Chigwada.
Wananchi wa Kata ya hogoro wanakabiliwa na changamoto ya uhaba wa wodi za wazazi pamoja na wahudumu afya na kuomba wadau kwa kushirikiana na serikali kuwaasaiidia kutatua adha hiyo.
Baadhi ya wananchi hao wakizungumza na taswira ya habari wamedai kukosekana kwa wodi za wazazi kujifungulia , vyumba vya mapumziko pamoja na uchache wa wahudumu wa afya imekuwa adha kwao huku baadhi ya vijiji vikiwa havina zahanati kabisa.
Mtendaji wa kijiji cha Nyerere Bi.Jema Mkada amekili kukosekana kwa huduma ya afya katika eneo lake hivyo wananchi kulazimika kufuata huduma zahanati ya kijiji jirani ambako nako wahudumu ni wawili
Naye Diwani wa Kata hiyo Bw.Mtwanga Samila amesema kuwa ni kweli kijiji cha Nyerere kinaukosefu wa zahanati hivyo kulazimika kupata huduma kijiji cha Hogoro huku zahanati zingine zikiwa na changamoto ya wahudumu
Licha ya uwepo wa zahanati katika vijiji mbalimbali nchini Serikali imeendelea kusisitiza na kuhakikisha kila Kata kuwa na kituo cha afya huku juhudi za kuajili watumishi zikiendelea