Dodoma FM

Jamii yatakiwa kutumia teknolojia za kisasa katika mapishi nyumbani ili kuepusha uharibifu wa mazingira

6 August 2021, 12:11 pm

Na; Benard Filbert.

Jamii inashauriwa kutumia teknolojia za kisasa katika matumizi ya kupika nyumbani na kuepuka kuharibu mazingira kitu ambacho ni hatari katika mabadiliko ya tabia ya Nchi.

Hayo yameelezwa na Marry Stanley kutokea taasisi ya Tanzania Traditional Energy Development TATEDO ambayo imekuwa ikijihusisha na utunzaji wa mazingira Nchini ambapo ameeleza kuwa kazi ya taasisi hiyo ni kuhamasisha jamii kutumia nishati ya gesi na umeme katika matumizi ya nyumbani.

Amesema lengo la kufanya hivyo ni kutokana na kukithiri kwa vitendo vya ukataji wa miti kwa ajili kutengeneza mkaa hivyo wamekuwa wakihamasisha kuachana na vitendo hivyo.

CLIP TATEDO……………01

Ameongeza kuwa ni vyema jamii ikaachana na upotoshaji kuwa matumizi ya vifaa vyenye teknolojia ya kisasa hususani kwenye nishati ya kupikia ni gharama kubwa kitu ambacho sio sahihi.

CLIP TATEDO……………….02

Serikali imekuwa ikihamasisha wananchi kutumia nishati mbadala ya kupikia majumbani haatua ambayo inatajwa kusaidia katika kuepusha uharibifu wa mazingira.