Mwitikio mdogo wa Elimu katika kata ya Farkwa wapelekea wanafunzi kushindwa kujiunga na masomo ya sekondari
1 July 2021, 12:48 pm
Na; Victor Chigwada.
Mwitikio mdogo wa elimu katika kata ya Farkwa Wilayani Chemba ni changamoto inayopelekea wanafunzi kushindwa kujiunga na masomo ya sekondari kwa shinikizo la wazazi.
Baadhi ya wazazi hao wakizungumza na taswira ya habari wamesema ni kweli suala hilo lipo kwa baadhi ya wazazi kuwashawishi watoto wao wajifelishe darasa la saba kwamadai kwamba hawana fedha za kuwaendeleza.
Mwenyekiti wa kijiji cha Bubutole Bw.Hosea Ndalami amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo inayotokana na shinikizo la wazazi kudai hawana fedha za kuwasomesha licha ya wanafunzi wenyewe kuwa na nia yakuendelea na masomo
Naye diwani wa Kata ya Farkwa Bw.Stephani Patrick amesema kuwa baadhi ya vijiji wazazi wengi wamekuwa hawana mwitikio katika suala la elimu hivyo kuwakatisha masomo watoto wao kwa lengo la kukwepa gharama.
Bw.Patrick ameongeza kuwa licha ya changamoto hiyo lakini pia mazingira ya shule yanachangia kukatisha masomo kwa baadhi ya watoto wa kike kupata ujauzito kwani baadhi ya wazazi hawataki watoto wao kuka shuleni
Kila mtoto anahaki ya kupata elimu kikatiba hivyo nijukumu la maafisa elimu wa kata kuhakikisha wanahamasisha umuhimu wa elimu katika maeneo ya vijijini