Wasichana wametakiwa kusoma kwa bidii masomo ya sayansi ili kupata fursa katika miradi inayo jitokeza
1 July 2021, 10:54 am
Na;Yussuph Hans.
Licha ya jitihada mbalimbali zinazofanyika kuleta usawa Nchini bado kuna Changamoto kwa wanawake katika kusomea Masomo ya Sayansi pamoja na kupewa fursa katika Miradi ya maendeleo ukilinganisha na Wanaume.
Akizungumza na Taswira ya habari Afisa Programu kutoka Mtandao wa Kijinsia Tanzania TGNP Flora Ndaba amesema kuwa Nguvu kubwa kwa sasa imeelekezwa katika kuwahamasisha Wasichana kusoma kwa Bidiii Masomo ya Sayansi ili kutengeneza Usawa katika Miradi inayojitokeza.
Baadhi ya Wanafunzi Mkoani Dodoma wamebainisha ukosefu wa Vitendea Kazi katika Masomo ya Sayansi kama Maabara na Vifaa vyake ni miongoni mwa sababu zinazopelekea kutokusoma masomo hayo.
Kwa upande wake Afisa elimu Jijini Dodoma Pendo Rwemamu amesema kwa kiasi kikubwa wamejitahidi kubadilisha dhana ya kuwa masomo ya sayansi ni magumu kwa wasichana, huku serikali ikiendelea na uboreshaji wa miundombinu ya kufundishia.