Serikali za mitaa na Mikoa zatakiwa kusimamia utekelezaji wa kanuni za usimamizi wa mazingira
29 June 2021, 12:38 pm
Na;Mindi Joseph.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Selemani Jafo amezitaka mamlaka za serikali za mitaa na Mikoa kusimamia utekelezaji wa kanuni za usimamizi wa mazingira katika udhibiti wa kelele na mitetemo ili kulinda afya za wananchi.
Akizungumza leo jijini Dodoma Waziri Jafo amesema kuwa Wakuu wa mikoa na wilaya wanatakiwa kusimamia kikamlifu sheria hiyo ya mwaka 2015 ya marufuku ya kelele ili Kuepuka kusababisha matatizo ya kiafya kwa wajawazito na watoto.
Waziri jafo ameongeza kuwa wananchi wanapaswa kufanya shughuli zao pasipo kusababisha kero kelele na mitetemo kwa wananchi wengine huku akiwataka Wamiliki wa kumbi za starehe na burudani kuhakikisha wanazingatia sauti za vipima kelele.
Kwa upande wake Waziri wa Afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Dkt Doroth Gwajima amesema Kelele na Mitetemo ni moja ya tatizo linalosababisha vifo na magonjwa kwani kwa mujibu wa utafiti barani ulaya watu 16,600 hupata vifo vya mapema
Aidha Wananchi wametakiwa kutoa taarifa za kero za kelele na mitetemo na Kwa atakayevunja sheria adhabu yake ni shilingi milion moja pamoja na kufungiwa kwa biashara yake husika ili kulinda afya ya wananchi .