Serikali yaombwa kutatua changamoto ya watumishi wa zahanati
24 June 2021, 8:15 am
Na; Victor chigwada
Wananchi wa mtaa wa Chololo Kata ya Kikombo jijini Dodoma wameiomba Serikali kuwatatulia changamoto ya uhaba wa watumishi kwenye zahanati na Shule ya msingi.
Wakizungumza na taswira ya habari baadhi ya wananchi hao wamesema pamoja na kupaza sauti kwa muda mrefu wakiomba kupatiwa ufumbuzi lakini bado changamoto hizo zimeendelea hali inayo rudisha nyuma maendeleo ya afya na elimu katika Kata yao.
Mwenyekiti wa mtaa Chololo Bw. Maiko Mbumi amesma wanaupungufu mkubwa wa watumishi wa afya pamoja na nyumba ya mganga mkuu huku upande wa elimu ikiwalazimu wazazi kuchangisha na kuwalipa walimu wa kujitolea.
Naye Diwani wa Kata ya Kikombo Bw.Emmanuely Manyono akitolea ufafanuzi changamoto hizo amesema tayari wapo kwenye mchakato wa kuanza kushughulikia ujenzi wa nyumba ya mganga mkuu huku suala la walimu wameshaliwasilisha kwa afisa elimu wa Wilaya kwa ajili ya atua zaidi.
Serikali imeendelea na juhudi za kuajiri watumishi katika kada mbalimbali zikiwemo afya, elimu na kadhalika.