Vikundi vya ukusanyaji taka vimetakiwa kufuata utaratibu ili kupunguza kero ya mrundikano wa taka mitaani
2 June 2021, 10:55 am
Na; Sani Nicolous.
Wito umetolewa kwa vikundi vya kukusanya taka katika maeneo mbalimbali jijini Dodoma kuzingatia utaratibu waukusanyaji taka uliowekwa na viongozi ili kupunguza kero zilizopo mtaani.
Akizungumza na Dodoma fm Afisa mazingira Bw. Dickson Kimaro amesema kuwa utaratibu ukifuatwa utatatua kero za ucheleweshwaji wa ukusanyaji taka katika baadhi ya maeneo jijini hapa.
Ameongeza kuwa kuna mpango wa kuongeza wazabuni wenye magari katika kata ya Ipagala ili kuondoa kero iliyopo maeneo hayo.
Dodoma fm imezungumza na meneja msaidizi wa greenwest Sedastiani Mkomagi ambaye amesema kuwa walikabidhiwa baadhi ya kata za kuzoa taka hivyo wapo tayari kufanya kazi kata yoyote ambayo mamlaka itapenda kuwaongezea lengo nikusaidia kuuweka mji wa Dodoma katika hali ya usafi .
Hii imefuatia baada ya wakazi wa Ilazo jijini Dodoma kulalmika ucheleweshwaji wa kuondolewa taka katika maeneo yao hali inayofanya mazingira yao kuwa machafu na kuhatarisha afya za wakazi hao.
Mazingira machafu ni chanzo cha kuzalisha wadudu wanaoweza kueneza magonjwa mbalimbali kama mbu , hivyo ni jukumu la kila mtu kuzingatia usafi ili kusaidiana na mamlaka ya afya kutokomeza magonjwa ya mlipuko kama kipindipindu.