Mrundikano wa taka wahatarisha maisha ya wakazi wa Ilazo
31 May 2021, 12:54 pm
Na; Shani Nicolous.
Wakazi wa mtaa wa Ilazo kati kata ya Ipagala jijini Dodoma wamelalamikia ucheleweshwaji wa uondoshaji wa taka takika mazingira yao hali inayosababisha kuzagaa kwa uchafu mtaani.
Wakizungumza na Dodoma fm wakazi hao wamesema kuwa kuna wakati taka zinakaa kwa zaidi ya mwezi mmoja nyumbani na kusabaabisha harufu mbaya na wadudu hali inayohatarisha afya zao.
Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa huo amesema kuwa baadhi ya wananchi hawatoi pesa kwa wakati ili kuondolewa taka hizo nahivyo kusababisha mrundikano
Wakati wakazi mtaa wa Ilazo wakilalamikia ucheleweshwaji wa kuchukuliwa taka hali hiyo ni tofauti na mtaa wa Ostabey ambapo wao wanabebewa taka kwa wakati hali inayofanya mazingira yao kuwa safii
Usafi ni jukumu la kila raia na hii ni kuanzia kwenye mwili wake , nyumbani na mazingira ya ofisini tabia hii ya usafi ni mbinu mojawapo ya kupunguza magonjwa ya mlipuko hivyo ni wajibu wa kila mtu kuzingatia usafi.