Uharibifu wa mazingira ni chanzo cha mabadiliko ya tabia Nchi
24 May 2021, 1:54 pm
Na;Mindi Joseph .
Uharibifu wa mazingira nchini umetajwa kuchangia kuongezeka kwa mabadiliko ya tabia nchi hali ambayo imepelekea kiwango cha maji kuzidi kuongezeka Nchini Tanzania.
Akizungumza jijini Dodoma leo Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh.Selemani Said Jafo amesema Dunia kwa sasa inakabiliwa na chanagmoto kubwa ya mazingira na kuchangia mabadiliko ya Tabia kuwa makubwa.
Amesema Tanzania imejipanga kufanya kampeni kabambe ya usafi na utuzaji wa mazigira ambayo itahusisha kila mtu,Mikoa,Wilaya na taasisi zote nchini ili kuendelea kutunza mazingira.
Waziri Jafo ameteua mabalozi Takribani 40 ambao watakuwa chachu ya kuhamasisha utuzaji wa mazingira kwa ajili ya kizazi cha sasa na kijacho.
Aidha Bali na uteuzi wa mabalozi hao waziri jaffo ameteua wajumbe wa kampeni ya utuzaji wa mazingira ambayo mwenyekiti wake ni Self Ally Self na uzinduzi wa kampeni hiyo unatarajia kufanyika June 5 mwaka huu ikibebwa na kauli mbiu isemayo “mazingira yangu Tanzania yangu naipenda Daima”.