Uhaba wa rasilimali fedha ulichangia kukwamisha mashindano ya Sayansi na teknolojia
13 May 2021, 11:46 am
Na; Benard Filbert.
Ukosefu wa rasilimali fedha umetajwa kuwa sababu iliyokuwa ikipelekea Wizara ya elimu sayansi na teknolojia kushindwa kufanya mashindano ya kitaifa ya sayansi teknolojia na ubunifu katika ngazi za Wilaya.
Hayo yameelezwa na profesa Kipanyula ambaye ni mkurugenzi wa sayansi , teknolojia na ubunifu kutoka wizara ya elimu sayansi na teknolojia wakati akizungumzia kilichokwamisha kufanyika kwa mashindano hayo ngazi ya Wilaya.
Amesema mashindano hayo yanahusisha makundi saba ikiwepo vyuo mbalimbali hivyo wizara inatazama jinsi ya kuanza utekelezaji wa suala hilo.
Kadhalika ameongeza kuwa wabunifu mbalimbali ambao wanapatikana kutokana na mashindao hayo, wizara inawaendeleza ili kuleta maslahi kwa jamii.
Mashindano ya kitaifa ya sayansi, teknolojia na ubunifu yanaandaliwa na wizara ya elimu sayansi na teknolojia lengo likiwa kuendeleza Sayansi, Teknolojia na Ubunifu kwa kuibua na kuendeleza wabunifu wachanga.