Wakazi wa mtaa wa Makulu waomba kuongezewa vifaa kwaajili ya kusafisha mazingira
10 May 2021, 1:19 pm
NA;Alfredy Sanga.
Viongozi wa Mtaa wa Makulu jijini Dodoma wameelezea changaoto wanazokutana nazo kila ifikapo mwisho wa mwezi wanapowaongoza wananchi kufanya usafi.
Akizungumza na Dodoma Fm balozi wa Mtaa wa Makulu Bw.Peter Salali amesema tangu kuanzishwa kwa utaratibu wa ufanyaji usafi kila ifikapo mwisho wa mwezi umesaidia mazingira mengi kuwa safi hali inayochangia kuepuka magonjwa ya mlipuko.
Amesema kuwa kwa sasa wanakabiliwa na changamoto za baadhi ya watu kujitokeza kufanya usafi pamoja na gari la kuzolea taka kutofika eneo hilo.
Nao baadhi ya wananchi wa Mtaa wa Makulu, wameeleza changamoto zinazosababisha kushindwa kujitokeza kufanya usafi wa mazingira kuwa ni pamoja na baadhi yao kuwa wavivu na kushindwa kushirikiana na wenzao.
Hata hivyo wananchi hao wameiomba Serikali kuwapa ushirikiano kwa kuwagawia vifaa vya usafi na kuwatengea eneo maalumu la kuhifadhi taka.