Vifungashio mbadala ni changamoto kwa wafanyabiashara Majengo
16 April 2021, 9:57 am
Na; Shani Nicolous.
Wafanyabiashara wa soko la majengo wamelalamikia kukosekana kwa vifungashio mbadala vilivyo elekezwa na Serikali vitumike .
Akizungumza na Taswira ya habari Mwenyekiti wa soko la Majengo Bw.Hamis Bomu amesema kuwa vifungashio mbadala vinavyo takiwa kutumika havipatikani kwa wakati na vichache vinavyo patikana huuzwa kwa bei kubwa ambayo wafanyabiashara wengi hawamudu kununua vifungashio hivyo.
Amesema kuwa ni vema viongozi wa serikali wanapo toa marufuku ya vitu basi wawe tayari wameandaa mbadala wa vitu hivyo mapema ili kuepusha adha inayoweza kujitokeza baada ya kukosekana na mbadala wa kitu kilicho pewa marufuku..
Aidha amewataka wafanyabiashara kutii amri ya serikali kwakuacha kutumia vifungashio vilivyokatazwa ilikuepuka faini zisizo za lazima na usumbufu mwingine.
Taswira ya habari haikuishia hapo ilipata nafasi ya kuzungumza na wafanyabiashara wa soko la Majengo ambapo wamesema vifungashio mbadala upatikanaji wake ni mdogo sana na hata wanapo vipata huwa wanauziwa kwa bei ghali hivyo wanaomba Serikali iwasaidie kupata vifungashio hivyo kwa urahisi.