Mfumuko wa bei wa Taifa washuka
8 December 2020, 2:51 pm
Na,Mindi Joseph,
Dodoma.
Mfumuko wa bei wa Taifa umepungua kutoka asilimia 3.1 hadi 3.0 kwa mwezi Novemba kufuatia kasi ya mabadiliko ya bidhaa nchini Kupungua.
Kupungua kwa mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba 2020 imechangiwa na kupungua kwa bei za bidhaa za vyakula ikilinganishwa na mwezi Novembar 2019.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii toka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bi.Lucy Minja, amesema mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi Novemba 2020 umepungua hadi asilimia 2.8 kutoka asilimia 3.4 kwa mwaka ulioishia mwezi oktoba 2020.
Wakati nchini Tanzania Mfumuko wa bei umepungua nchi za afrika mashariki mfumuko wa bei nchini kenya umeongezeka hadi asilimia 5.46 wakati nchini uganda umepungua hadi asilimia 3.7 kwa mwezi novembar 2020.
Mfumuko wa bei wa Taifa unapima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafisi.