Dodoma FM
Dodoma FM
04/03/2026, 16:48

Msaada huo umetolewa kama chachu ya wanafunzi wenye mazingira magumu kutimiza ndoto zao za kimasomo.
Na Steven Noel.
Shirika la HakiElimu limetoa msaada wa sare za shule na vifaa vingine vya kujifunzia kwa wanafunzi waishio katika mazingira magumu wilayani Mpwapwa.
Akiongea wakati wa kukabidhi msaada huo Afisa Elimu kata ya Mazae Bi Honaratha Viane amesema msaada huo umetolewa ukawe chachu ya wanafunzi hao kutimiza ahadi zao za masomo .