Dodoma FM
Dodoma FM
23 February 2026, 5:08 pm

Inatarajiwa kupokea zaidi ya kontena 1500, jambo litakalorahisisha biashara na kuongeza kasi ya usafirishaji wa bidhaa ndani na nje ya nchi.
Na Mariam Kasawa.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule, amefanya ziara ya kukagua mradi wa Bandari Kavu Ihumwa, Ni hatua ya kimkakati itakayobadilisha taswira ya uchumi wa mkoa na taifa kwa ujumla.
Bandari hii mpya itakuwa suluhisho la msongamano wa Bandari ya Dar es Salaam kwa kupokea na kusafirisha mizigo kwa ufanisi zaidi.
Zaidi ya kupunguza msongamano, mradi huu ni kiungo cha kimkakati cha uchumi wa taifa. Utaleta ajira mpya,kuongeza mapato ya Mkoa na kuifanya Dodoma kuwa kitovu cha biashara na uwekezaji.