Dodoma FM
Dodoma FM
12 February 2026, 4:37 pm

Vile vile afisa huyo ametoa rai kwa wananchi kutosita kutoa maoni pamoja na taarifa pindi wanapoona kuna viongozi wanakiuka misingi ya maadili ya umma na hatua za kisheria kuchukuliwa dhidi ya kiongozi au viongozi hao.
Na Jerome John.
Viongozi wa umma nchini wametakiwa kuonesha maadili mema kwa wananchi wanao waongoza ili kulinda misingi ya utumishi bora katika jamii.
Wito huo umetolewa na Anno Mgani afisa kutoka ofisi ya sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma nchini,wakati akizungumza na Taswira ya Habari juu ya kukuza na kusimamia maadili nchini.
Afisa huyo amebainisha kuwa viongozi wa umma wanawajibu wa kuhakikisha misingi ya maadili inatekelezwa ipasavyo na wao kuwa kioo kwa wananachi wanaowaongoza ili kujenga taifa lenye watu wenye maadili bora.
Aidha bwana Anno amewasisitiza wazazi,walezi,viongozi wa dini pamoja na viongozi wa jadi kuhakikisha wanakemea suala la uvunjifu wa maadili katika jamii na kuchukua hatua ili nchi irudi katika misingi ya maadili bora na kuwa na viongozi wenye maadili.