Dodoma FM

Nyumba zilizopanda miti Iyumbu zakabidhiwa vyeti

10 February 2026, 12:14 pm

Picha ni mkuu wa Mkoa wa Dodoma mh. Rosemery Senyamule akishiriki kupanda mti katika hafla hiyo.Picha na Mkoa wa Dodoma.

Amewasisitiza wananchi kuzingatia sheria ya kuzuia mifugo kuzurura ovyo mitaani kwnai inachangia kwa kiasi kikubwa uharibifu wa mazingira.

Na Mariam Kasawa.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule, amekabidhi vyeti kwa kaya zilizofanya vizuri kwenye zoezi la upandaji miti nyumba kwa nyumba wakati wa uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti katika Kata ya Iyumbu, iliyoandaliwa na Umoja wa Wananume wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika Mteule wa Iyumbu Jijini Dodoma .

Akiongea katika hafla hiyo mkuu wa mkoa wa Dodoma Mhe. Senyamule amesema, utunzaji wa mazingira unahitaji usimamizi wa karibu wa Viongozi wa Serikali katika ngazi husika kuanzia Vijiji, Kata, Wilaya, Mkoa hadi Taifa kwa ujumla.

Aidha amewasisitiza wananchi kuzingatia sheria ya kuzuia mifugo kuzurura ovyo mitaani kwnai inachangia kwa kiasi kikubwa uharibifu wa mazingira.

Sauti ya mh. Senyamule