Dodoma FM
Dodoma FM
30 January 2026, 2:29 pm

Picha ni Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi akifungua Baraza Kuu la 55 la Wafanyakazi wa TANESCO. Picha na Wizara ya Nishati.
Serikali imeweka malengo ya kuhakikisha angalau 80 % ya kaya za Tanzania zinatumia nishati safi ya kupikia kufikia mwaka 2034 kama ilivyoelekezwa katikaMkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia (2024–2034).
Na Victor Chigwada.
Imeelezwa kuwa endapo elimu ya matumizi ya nishati safi itaendelea kutolewa kwa wananchi hususani vijijini itasaidia wananchi kuepukana na uharibifu wa mazingira ikiwemo ukataji wa miti ovyo.
Hayo yameelezwa na baadhi ya wananchi wa kijiji cha Mnase wilayani Chamwino, mkoani Dodoma ambapo wamesema kijijini hapo wanakabiliwa na janga la ukataji miti hovyo kutokana na watu wengi kufanya biashara ya mkaa na kuni.
Naye Mwenyekiti wa kijiji cha Mnase Bw. Ayubu Malima amesema kuwa ili kukabiliana na changamoto ya uharibifu wa mazingira wameendelea kutoa elimu kwa wananchi hao ili kuhakikisha wanakuwa na mazingira salama ikiwa ni pamoja na kuweka kanuni ndogondogo Kwa lengo la kupunguza uvamizi wa mapori.