Dodoma FM

Waziri Mkuu aonya kupandisha bei za vyakula

29 January 2026, 2:18 pm

Picha ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Chemba, Bungeni jijini Dodoma. Picha na Wizara ya Afya.

Dkt. Mwigulu amesema pia kuwa serikali kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) inaendelea kusambaza chakula katika maeneo yenye uhitaji ili kuhakikisha Watanzania wanapata chakula cha kutosha.

Na Mariam Kasawa.

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, amewaagiza wafanyabiashara wa vyakula nchini kutotumia vipindi vya mfungo wa Ramadhani na Kwaresma kuongeza bei kwa kisingizio cha upungufu wa chakula.

Akizungumza Bungeni jijini Dodoma leo Januari 29, 2029, wakati wa Kipindi cha Maswali ya Papo kwa Papo kwa Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu amesema kuwa licha ya tahadhari kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kuhusu uhaba wa mvua, nchi haina uhaba wa chakula na kuna ziada ya kutosha.

Waziri Mkuu alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Nancy Nyalusu, aliyetaka kufahamu mipango ya serikali katika kuhakikisha uhaba wa chakula haujitokezi wakati wa mfungo wa Kwaresma na Ramadhani.

Sauti ya Dkt. Mwigulu Nchemba.