Dodoma FM
Dodoma FM
29 January 2026, 2:04 pm

Picha ni Waziri wa Kilimo, Mhe. Daniel Chongolo akikabidhi vitendea kazi vyenye thamani ya shilingi bilioni 23.4 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya Umwagiliaji. Picha na Wizara ya Kilimo.
Sekta ya kilimo imeendelea kuwa muhimili muhimu wa kilimo, ambapo takribani 65% ya nguvu kazi ya nchi inategemea kilimo kwa ajira yao, ikimaanisha sekta hii inawasaidia watanzania wengi kupata kipato.
Na Lilian Leopold.
Elimu ya kilimo inayotolewa na wataalamu wa masuala ya kilimo imeendelea kuleta tija kwa wakulima nchini, baada ya kuwasaidia kuboresha uzalishaji na kuinua maisha yao kupitia matumizi ya njia bora na sahihi za uandaaji wa shamba.
Njia hizo ni pamoja na kusafisha mashamba ipasavyo, matumizi sahihi ya mbolea pamoja na upimaji wa udongo kabla ya kilimo, hatua ambazo zimeongeza uzalishaji na kupunguza hasara kwa wakulima wengi.

Kwa mujibu wa ripoti ya Annual Agricultural Sample Survey (AASS) ya mwaka 2023/2024 kilimo kinaendelea kuwa sekta kuu ya uchumi wa Tanzania na kuchangia takribani 26.5% ya pato la Taifa, jambo linaloonesha umuhimu wa kuendelea kuwekeza katika elimu ya kilimo na matumizi ya teknolojia na mbinu za kisasa.
Lilian Leopold amezungumza na Mtaalam wa kilimo kutoka kampuni ya Josasa Farms Jofrey Samwel iliyopo Nzunguni jijini Dodoma ili kufahamu wanafanyaje kuhakikisha wanawasadia wakulima kuweza kutumia njia bora katika kilimo.