Dodoma FM
Dodoma FM
28 January 2026, 2:47 pm

Picha ni Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi na baadhi ya wazee wakipanda miti. Picha na Mariam Matundu.
Zoezi la upandaji Miti mbele ya Ofisi ya Waziri Mtumba Jijini Dodoma limehusisha Kundi la Wazee Mkoa wa Dodoma, Menejimenti na Watumishi wa Wizara hiyo.
Na Mariam Matundu.
Baraza la Wazee Mkoawa Dodoma limeshirikiana naWizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum katika upandaji miti ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya kuzaliwa kwa Rais wa Jamhuri yaMuunganowa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mhe. Dkt. Samia aliamua kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa kwa vitendo kwa kupanda mti ikiwa na lengo la kulinda na kuhifadhi mazingira.
Wakizungumza mara baadaya zoezi hilo wazee hao wamempongeza Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uongozi wake mahiri na thabiti katika kuliongoza taifa kwa misingi ya amani na utulivu.
Akiongoza zoezi hilo Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi Januari 27, 2026 amesema lengo ni kuenzi maono ya Rais Samia la kutunza mazingira yanayotuzunguka.
Naibu Waziri Mahundi amempongeza Rais Dkt. Samia kwa uongozi wake kwa kuendelea kudhihirisha kiongozi maono, mbunifu wake na namna anavyojali maslahiya Taifa.
Naye Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. John Jingu amesemaWizara imeshirikiana na kundi la Wazee kuwakilisha Makundi Maalum yanayosimamiwa na Wizara katika zoezi hilo ambalo lina lengo la kulinda na kutunza mazingira.