Dodoma FM
Dodoma FM
28 January 2026, 12:38 pm

Picha ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Dodoma, Sakina Mbugi akipanda mti katika shule ya msingi Mbwanga, jijini Dodoma. Picha na Lilian Leopold.
Zoezi la upandaji wa miti limefanyika katika maeneo mbalimbali ya jiji ikiwemo shuleni, taasisi za umma na maeneo ya makazi.
Na Lilian Leopold.
Jiji la Dodoma limeendelea kutekeleza kampeni ya upandaji miti ikiwa ni sehemu ya juhudi ya kuhifadhi mazingira na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi, huku wananchi wakihimizwa kujenga utamaduni wa kupanda na kutunza miti ili kulinda mazingira na kuhakikisha ustawi wa vizazi vijavyo
Akizungumza katika zoezi hilo lililofanyika katika shule ya msingi Mbwanga Katibu Tawala wa Wilaya ya Dodoma, Sakina Mbugi amesema kampeni ya upandaji wa miti ni kulifanya jiji la Dodoma kuwa kijani na kuungana mkono jitihada za serikali katika utunzaji wa mazingira.

Miongoni mwa walioshiriki katika zoezi hilo ni Diwani wa Kata ya Mnadani,Mugendi Kerenge na Mwenyekiti wa mtaa wa Mnadani Hema Wawa wamesema ni jukumu la kila mwananchi kutunza mazingira hivyo zoezi hilo litakua endelevu katika kata hiyo.
Jumla ya miti 150 imepandwa katika shule ya msingi Mbwanga, ambapo zoezi hilo limeshirikisha viongozi wa serikali ya mtaa, wanafunzi na wananchi.